1 Peter 2:5-9

5 aninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mnajengwa kuwa nyumba ya kiroho, ili mpate kuwa ukuhani mtakatifu, mkitoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. 6 bKwa maana imeandikwa katika Maandiko:

“Tazama, naweka katika Sayuni,
jiwe la pembeni teule lenye thamani,
na yeyote atakayemwamini
hataaibika kamwe.”
7 cKwenu ninyi mnaoamini, jiwe hili ni la thamani. Lakini kwao wasioamini,

“Jiwe walilolikataa waashi
limekuwa jiwe kuu la pembeni,”
8 dtena,

“Jiwe lenye kuwafanya watu wajikwae,
na mwamba wa kuwaangusha.”
Wanajikwaa kwa sababu hawakulitii lile neno, kama walivyowekewa tangu zamani.

9 eLakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki ya Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.
Copyright information for SwhNEN